Skip to main content Accessibility help
×
Hostname: page-component-55f67697df-sqlfs Total loading time: 0 Render date: 2025-05-09T00:24:53.486Z Has data issue: false hasContentIssue false

51 - Vyote Ving’aavyo Si Dhahabu

Published online by Cambridge University Press:  17 April 2025

Get access

Summary

  • 1. Tofauti ya dhahabu na madini mengine

  • 2. Matumizi ya methali hii katika mambo mengine ya maisha

  • 3. Methali yenyewe yasemaje

  • 4. Tusidharau kutahadhari

  • 5. Sura mbaya kwa nje

Tamthili ya methali zote methali hii ni matokeo ya maarifa barabara.

Dhahabu ni madini bora ing’aayo. Lakini kwa hili hatuwezi kusema kwamba kila king’aacho ni dhahabu. Kitu king’aacho huweza kuwa dhahabu au huweza kuwa si dhahabu. Methali hii yasema kwamba tusifikiri vitu vyote ving’aavyo kuwa dhahabu. Kuna madini zing’aazo kama dhahabu lakini hazina maana. Shaba iliyokwatuliwa, madini zilizoghushiwa na dhahabu za kuiga hung’aa kama dhahabu; lakini si dhahabu. Mng’ao wa madini una hadaa mara kwa mara, hivyo tungeangalia sana katika kupambanua dhahabu na shaba, madini zote mbili zing’aapo.

Methali hii husema kweli katika mambo mengine ya maisha. Kuna watu wengi waonekanao kuwa wastaarabu na bora. Lakini kwa kweli ni maayari. Waweza kudhani mtu aliyevaa libasi nzuri kuwa tajiri; lakini kwa kweli aweza kuwa maskini. Katika nguo vile vile hariri ya kuiga hufanana na hariri halisi, na kama hatuangalii, twapunjwa. Ukinunua kitabu kwa sababu kina jalada zuri tu, utajuta mara moja. Katika sanaa vile vile, sanaa zisizo maana huonekana mara kwa mara nzuri kama sanaa hasa. Lakini lazima tupambanue baina ya vitu hivi viwili. Hali hii hii imo katika vitu vya chakula. Uto wa nyama hufanana sana na samli safi. Basi kama huangalii, mfanyabiashara hukupunja kwa kukupa uto wa nyama kwa kukutoza thamani ya samli.

Methali yenyewe yasema kwamba sura huhadaa mara kwa mara. Kwa hivi tusitegemee sura nzuri tupu, lakini lazima tujaribu kugundua ubora wa watu au vitu. Yatuonya kuangalia katika kupambanua chema na kibaya, dhahabu na shaba na nafaka na kapi. Kama hatuangalii katika jambo hili, itatupasa kujutia uchaguzi wetu mbaya.

Lazima tutie sana maanani methali hii, lakini tusikithiri kujihadhari. Ingawa vyote ving’aavyo si dhahabu, vyote ving’aavyo si shaba. Kwa hivi tusituhumu kila kitu king’aacho. Kama uzembe katika kupambanua vitu au watu ni kosa, kukithiri kujihadhari katika jambo ni kosa vile vile. Tukituhumu mara kwa mara ubora wa mtu au kitu, maendeleo yetu yatakoma. Maisha yametegemea tumaini na uthabiti. Hivyo tusidhani mtu yeyote au kitu chochote kuwa hakina maana mwanzoni.

Type
Chapter
Information
Kielezo cha Insha , pp. 95 - 97
Publisher: Wits University Press
Print publication year: 2024

Access options

Get access to the full version of this content by using one of the access options below. (Log in options will check for institutional or personal access. Content may require purchase if you do not have access.)

Save book to Kindle

To save this book to your Kindle, first ensure [email protected] is added to your Approved Personal Document E-mail List under your Personal Document Settings on the Manage Your Content and Devices page of your Amazon account. Then enter the ‘name’ part of your Kindle email address below. Find out more about saving to your Kindle.

Note you can select to save to either the @free.kindle.com or @kindle.com variations. ‘@free.kindle.com’ emails are free but can only be saved to your device when it is connected to wi-fi. ‘@kindle.com’ emails can be delivered even when you are not connected to wi-fi, but note that service fees apply.

Find out more about the Kindle Personal Document Service.

Available formats
×

Save book to Dropbox

To save content items to your account, please confirm that you agree to abide by our usage policies. If this is the first time you use this feature, you will be asked to authorise Cambridge Core to connect with your account. Find out more about saving content to Dropbox.

Available formats
×

Save book to Google Drive

To save content items to your account, please confirm that you agree to abide by our usage policies. If this is the first time you use this feature, you will be asked to authorise Cambridge Core to connect with your account. Find out more about saving content to Google Drive.

Available formats
×