Palitokea shindano la wanawake juu ya kueleza uzuri wao katika nchi ya hewa ya manukato, ardhi ya kioo mito ya marashi na makonde ya mapambo. Nchi hiyo ilikuwa ndoto kubwa ya wanawake kwa sababu kila mwanamke alijali sana manukato na mapambo kuliko wakati wake, tena alipenda sana kioo kuliko kazi yake. Washindani walikuwa Mnene kwa ajili ya wanawake wanene, Mwembamba kwa ajili ya wanawake wembamba, Mweupe kwa ajili ya wanawake weupe, na Mweusi kwa ajili ya wanawake weusi. Kwa kuwa silaha kubwa ya mwanamke ilikuwa ulimi wake, kila mshindani alikuwa msemaji mwema katika shindano
Mnene alijitangaza, “Katika wanawake wazuri ulimwenguni hapatikani mwanamke wa kushindana na mimi. Angalia, nina afya na nguvu! Uzuri wa kwanza mwilini ni afya, nami ninayo ya kutosha. Kwa nguvu yangu, naweza kufanya kazi yoyote ngumu itakiwayo. Mimi ni fahari ya wanawake katika dunia.”
Mwembamba alinena, “Uzuri wangu haulingani na wa mwanamke yeyote katika dunia hii ya haraka na wepesi. Wembamba si udhaifu. Ni umbo la ajabu liwezalo kutenda miujiza bila kutoka jasho. Nina wepesi na haraka katika matendo yangu. Baadhi ya kazi hutaka akili, nami ninayo kwa wingi. Mimi ni bora katika mabibi.”
Mweupe alisema, “Mimi ni nuru katika wanawake kama jua lilivyo katika mbingu na dunia. Jua mfalme wa sayari, binti yake ni mimi. Kwa hivi uzuri wangu haushindwi na wa mwanamke yeyote. Nashika macho ya ulimwengu mzima katika mkono wangu mmoja. Furaha ya dunia imo katika miliki yangu.”
Mweusi alitamka, “Mimi ni bora katika wanawake. Weusi si uchafu. Ni aina moja ya maumbile, nayo ina uzuri wake. Kwa weusi wangu nimekuwa taji juu ya kila kichwa cha mtu. Ukitazama katika nywele, nyusi, kope na mboni za macho ya watu utaona rangi yangu. Kurasa za vitabu vikubwa duniani zimeandikwa kwa wino mweusi. Mimi ni malkia wa uzuri katika wanawake.”
Kama ulikuwa mmoja wa waamuzi katika shindano hili, ungalimpa ushindi mwanamke gani?
To save this book to your Kindle, first ensure [email protected] is added to your Approved Personal Document E-mail List under your Personal Document Settings on the Manage Your Content and Devices page of your Amazon account. Then enter the ‘name’ part of your Kindle email address below. Find out more about saving to your Kindle.
Note you can select to save to either the @free.kindle.com or @kindle.com variations. ‘@free.kindle.com’ emails are free but can only be saved to your device when it is connected to wi-fi. ‘@kindle.com’ emails can be delivered even when you are not connected to wi-fi, but note that service fees apply.
Find out more about the Kindle Personal Document Service.
To save content items to your account, please confirm that you agree to abide by our usage policies. If this is the first time you use this feature, you will be asked to authorise Cambridge Core to connect with your account. Find out more about saving content to Dropbox.
To save content items to your account, please confirm that you agree to abide by our usage policies. If this is the first time you use this feature, you will be asked to authorise Cambridge Core to connect with your account. Find out more about saving content to Google Drive.