Book contents
- Frontmatter
- Contents
- Preface
- Acknowledgements
- Chronology
- Photographic Section
- Introduction: Ngũgĩ wa Thiong'o: Reflections on His Life of Writing
- Ngũgĩ at Work
- Part I Serenades & Beginnings
- Part II Memories, Recollections & Tributes
- Part III Working with Ngũgĩ
- Part IV The Writer, the Critic & the World
- Part V The Other Ngũgĩ
- 31 Kwa Grant Kamenju: Hotuba ya Kuipokea Digrii ya Heshima ya Uzamifu Kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
- 32 Wasomi, Lugha za Ulaya na za Kiafrika: Kati ya Kuweza na Kuwezwa
- 33 Asia in My Life
- 34 Ndaĩ ya Wendo (A Riddle of Love)
- Appendixes
- References
- Bibliography of Ngũgĩ's Primary Works
- Works Cited
- Notes on Contributors
- Index
32 - Wasomi, Lugha za Ulaya na za Kiafrika: Kati ya Kuweza na Kuwezwa
from Part V - The Other Ngũgĩ
Published online by Cambridge University Press: 27 July 2019
- Frontmatter
- Contents
- Preface
- Acknowledgements
- Chronology
- Photographic Section
- Introduction: Ngũgĩ wa Thiong'o: Reflections on His Life of Writing
- Ngũgĩ at Work
- Part I Serenades & Beginnings
- Part II Memories, Recollections & Tributes
- Part III Working with Ngũgĩ
- Part IV The Writer, the Critic & the World
- Part V The Other Ngũgĩ
- 31 Kwa Grant Kamenju: Hotuba ya Kuipokea Digrii ya Heshima ya Uzamifu Kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
- 32 Wasomi, Lugha za Ulaya na za Kiafrika: Kati ya Kuweza na Kuwezwa
- 33 Asia in My Life
- 34 Ndaĩ ya Wendo (A Riddle of Love)
- Appendixes
- References
- Bibliography of Ngũgĩ's Primary Works
- Works Cited
- Notes on Contributors
- Index
Summary
(Mhadhara wa hadhara uliotolewa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Ukumbi wa Nkrumah, baada ya kutunukiwa Digrii ya Heshima ya Uzamifu [PhD] na Chuo hicho, 23 Novemba, 2013)
Katika mhadhara huu, nataka kuangalia na kufafanua, kwa ufupi tu, uhusiano wa kitaaluma kati ya lugha za Afrika na za Ulaya, na hasa Kiingereza. Jambo hili ni muhimu katika wakati huu, ambapo nchi nyingi za Afrika zinasherehekea miaka hamsini tangu zipate uhuru wake kutoka utawala wa kikoloni.
Msomi, au mwanataaluma wa aina yoyote ile, si kitu kipya kwa Afrika: Kila jamii, za leo au za kale, zilikuwa na wasomi au wanataaluma wake. Tunalitumia hili neno ‘msomi’ kwa maana ya mtu anayeshughulika na fikira. Yawezekana kwamba msomi huyo huenda akawa ana ujuzi mwingine; lakini kazi yake kuu inayojitokeza ni matokeo ya kujishughulisha kwake na fikira. Katika kundi hili wanaingia pia waganga wa kimwili na wa kiroho, wahunzi (au wafua vyuma), wajenzi, na mafundi wengineo.
Watu kama hawa walikuwa ni miongoni mwa wajenzi wa utamaduni wa Misri, Uhabeshi, Zimbabwe, Songhai, na kwengineko. Kati ya hao, alikuwamo pia mshairi, ambaye alichanganya ujuzi wa historia, maadili na utabiri. Afrika ya Magharibi, mtu kama huyo aliitwa ‘griot’. Uswahilini kulikuwa na washairi wengi waliokuwa ni viongozi wa fikira, na ambao wameendelea kuweko karne baada ya karne. Kitabu alichokihariri Abdilatif Abdalla, na kuchapishwa na shirika la Mkuki na Nyota, kiitwacho Kale ya Washairi wa Pemba: Kamange na Sarahani, kina majina ya wachache kati ya hao. Miongoni mwao wakiwemo Fumo Liyongo wa Bauri (karne ya kumi na mbili); Zahidi Mgumi (karne ya kumi na nane); Muyaka bin Haji; Suud bin Said al-Maamiriy; Kamange na Sarahani (wote ni wa karne ya kumi na tisa); na wengineo walioishi katika karne ya ishirini. Washairi kama hawa walikuwa ni sauti za jamii zao, na pia watetezi wa haki. Ni muhimu kueleza hapa kwamba washairi-wasomi kama hao – tangu hizo zama za ustaarabu wa Misri, mpaka katika ustaarabu wa Waswahili – walitumia lugha za jamii zao. Yaani wasomi wa kabla ya kuvamiwa na utawala wa kikoloni, walikuwa wameshikamana na mizizi ya jamii zao.
Leo nataka kuzungumza, kwa ufupi tu, kuhusu msomi Mwafrika wa zama zetu.
- Type
- Chapter
- Information
- NgugiReflections on his Life of Writing, pp. 186 - 193Publisher: Boydell & BrewerPrint publication year: 2018
- 1
- Cited by